Saturday, July 27, 2019

Mahakama: Ruhusa kwa Trump kutumia fedha za jeshi kujenga ukuta

Ukuta wa mpakaniHaki miliki ya pichaEPA
Mahakama kuu nchini Marekani imesema kuwa Raisi Donald Trump anaweza kutumia pauni bilioni mbili. fedha za idara ya ulinzi kwa ajili ya sehemu ya gharama za ujenzi wa ukuta wa mpaka wa kusini.
Mahakama imetoa uamuzi huo kwa ushindi wa kura tano kwa nne kuzuia hukumu ya jaji wa jimbo la California ambaye alimzuia raisi kutumia kiasi hicho cha fedha kwa kujenga ukuta.
Ukuta, unaotenganisha Marekani na Mexico, ilikuwa kampeni kubwa ya Trump, ahadi aliyoitoa kwenye wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2016.
Lakini mpango huo ulipingwa vikali na Democrats.
Uamuzi wa mahakama kuu unamaanisha kuwa fedha zitatumika kwa ajili ya miradi ya ukuta katika jimbo la California, Arizona na New Mexico.
Mahakama ya California ilidai kuwa bunge la Congress halikuidhinisha fedha hizo mahususi kwa ajili ya matumizi ya ujenzi wa ukuta.
Katika ukurasa wake wa twitter, bwana Trump amesema uamuzi huo ni ''ushindi mkubwa''
Raisi amedai kuwa ukuta mpya utasaidia kupambana na uhamiaji haramu, ambao amesema umekuwa mchango kwa kuchochea uhalifu na kuzorotesha uchumi.
Wabunge wa Democrat wamesema wanaunga mkono suala la usalama wa mipaka lakini ujenzi wa ukuta ni gharama kubwa na si njia ya kupata suluhu. 
Siku ya Ijumaa, Marekani na Guatemala walitia saini makubaliano, ambayo yatafanya wahamiaji kutoka Honduras na El Salvador wanaopitia Guatemala kuanzia kuomba hifadhi nchini Guatemala kwanza, kabla ya moja kwa moja kuingia Marekani.
Uamuzi umepokewaje?
Spika wa bunge Nancy Pelosi amesema: ''Jioni hii uamuzi wa mahakama ya juu kumruhusu Donald Trump kuiba fedha za jeshi na kuzipoteza kwenye ukuta, mpango ambao bunge halikuunga mkono ni jambo la udhaifu kabisa.Waasisi wetu waliweka misingi ya demokrasia ya watu- na si ufalme.''
Asasi ya kiraia ya The American Civil Liberties Union (ACLU) imeapa kupata uamuzi wa haraka kwenye mahakama ya rufaa ''dhidi ya mpango wa Trump''.
Gloria Smith, wakili wa wanaharakati wa mazingira ambao wamekuwa wakipinga mpango huo amesema: ''Uamuzi wa leo kuruhusu fedha za jeshi kujenga ukuta wa mpaka utatenganisha na kuharibu jamii, aridhi za watu na maji jimboni California, New Mexico na Arizona.''
Raisi TrumpHaki miliki ya pichaEPA
Trump alitangaza hali ya dharura mwanzoni mwa mwaka huu, akisema anahitaji dola bilioni 6.7 kujenga ukuta kwa ajili ya ulinzi wa usalama wa taifa. Hatahivyo kiasi hicho ni kidogo sana ikilinganishwa na makadirio ya dola bilioni 23 kwa ajili ya mpaka wa umbali wa kilomita 3,200.
Wabunge wa democrat walidai kuwa uamuzi wa Trump kutangaza hali ya dharura alizidisha mamlaka yake kwa mujibu wa katiba ya Marekani.
Majimbo takriban 20, sambamba na wanaharakati wamefungua shauri kujaribu kumzuia raisi kutumia dharura kuruka mamlaka ya congress.
Makundi ya wanaharakati wa mazingira wamekuwa katika kampeni ya kupinga jitihada za Trump wakidai kuwa ujenzi wa ukuta utaleta athari kwa wanyama pori.
Bunge la wawakilishi pia linachukua hatua za kisheria kuzuia fedha zaidi kutolewa kwa ajili ya mradi wa ukuta.

Kinachoendelea mpakani.

Kwa mujibu wa mamlaka za nchini Marekani, watu 104,344 walikamatwa katika mpaka wa kusini magharibi mwezi Juni- idadi iliyopungua kwa asilimia 28 ikilinganishwa na mwezi wa tano.
Utawala wa Trump umedai kuwa kupungua kwa idadi hiyo ni kutokana na sera mpya zilizowekwa ili kupambana na uhamiaji, ikiwemo kuongeza ulinzi wa mpaka wa upande wa Mexico na mpango wa kuwasubirisha nchini Mexico watu wanaotafuta hifadhi wakati maombi yao yakifanyiwa kazi. 
Ripoti ya Umoja wa mataifa kuhusu wahamiaji wasiojulikana walipo imeripoti kuwa wahamiaji 170 wamepoteza maisha au kupotea kwenye mpaka wa Marekani na Mexico mpaka sasa wakiwemo watoto 13.
Idara ya usalama imesema ''bado tunakabiliwa na changamoto ya usalama mpakani na masuala ya kibinaadamu''.

Monday, July 22, 2019

Rais Adama Barrow asema huenda asijiuzulu Gambia baada ya miaka mitatu

Mnamo 2016, raia nchini Gambia waliouonyesha ulimwengu nguvu ya demokrasia wakati walipomtimua rais Yahya Jammeh kupitia uchaguzi. Sasa kuna wasiwasi kuwa rais mpya nchini humo Adama Barrow, huenda pia akajaribu kung'angania uongozi. Ameiambia BBC Africa Eye hatotii makubaliano ya kujiuzulu baada ya miaka mitatu na anafikiria kushiriki katika uchaguzi ujao.

Thursday, July 18, 2019

Iran: Meli ya kigeni yakamatwa ikisafirisha mafuta 'kimagendo' Ghuba

File photo showing Iranian Revolutionary Guards naval vessels during a ceremony near Bandar Abbas on 2 July 2012Haki miliki ya pichaAFP
Iran inasema kuwa imekamata meli ya kigeni ya mafuta na wafanyikazi wake 12 ikisafirisha ''kimagendo'' mafuta kati eneo la Ghuba siku ya Jumapili.
Runinga ya kitaifa imewanukuu maafisa wa jeshi la majini wakisema kuwa meli hiyo ilikuwa na lita milioni moja ya mafuta.
Haijathibitishwa ikiwa meli hiyo ni ile inayomilikiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE- ambayo ilipoteza mawasiliano ikiwa katika bahari ya Strait of Hormuz Jumapili.
Mapema wiki hii Iran ilisema kuwa iliisaidia meli iliyoharibika katika eneo lake bila kutaja jina la meli hiyo, na kuongeza kuwa iliivuta kutoka majini kwenda kuikarabati baada ya ''kupokea ombi al usaidizi''
Hali ya taharuki imekuwa ikishuhudiwa katika eneo la Ghuba tangu Marekani ilipoiwekea upya vikwazo vilivyolenga sekta yake ya mafuta na kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015.
Map of the Strait of Hormuz
Katika kujibu hatua hiyo, Iran ilitangaza mwezi Julai kuwa imeongeza kiwango cha urutubishaji wa madini ya urani yaliyowekwa kwenye makubaliano hayo.Nchi hiyo imesisitiza kuwa haijaribu kutengeneza silaha za nyukilia.
Katika mahojiano ya televisheni siku ya Jumatatu, Bwana Zarif amesema kwenye televisheni ya NBC kuwa nafasi ya mazungumzo ipo wazi'' ikiwa Marekani itaondoa vikwazo.
Raisi wa Marekani Donald Trump amesema Marekani ''imepiga hatua'' na Iran na kuwa hawakuwa ''wakitafuta kuubadili utawala'', ingawa alisisitiza kuwa nchi haiwezi kutengeneza silaha za nyukilia na haiwezi kujaribu makombora ya masafa marefu.
Mapema mwezi Mei, Trump aliweka shinikizo zaidi kwa Iran kwa kuidhinisha upya marufuku kwa matiafa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.
Hatua hiyo ilinuiwa kusitisha kipato kikuu kwa serikali ya Iran.
Donald Trump akiwa ameshika waraka aliotia saini kujiondoa kwenye mkataba wa nyukilia wa IranHaki miliki ya pichaEPA
Kwanini Iran imeongeza viwango vya urutubishaji?
Rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kuwa nchi yake inarudi nyuma katika ahadi zake katika makubaliano hayo.
Hii ikiwa ni pamoja na kutotiii sheria kuhusu akiba yake ya urutubishaji mdogo wa madini ya Uranium kiwango kilichowekwa kikwa ni - 300kg na tani 130 - na kusitisha uuzaji wa akiba ya ziada katika mataifa ya nje.
Rouhani pia aliyapatia mataifa hayo ya Ulaya siku 60 kulinda mauzo ya mafuta ya Iran. Iwapo yatashindwa kufanya hivyo , Iran itakiuka masharti ya urutubishaji Uranium na kusitisha uundwaji upya wa kinu cha Arak, ambacho mafuta yake yaliotumika yana plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.
Marekani imekuwa ikiilaumu Irana kwa kuhusika na mashambulio dhidi ya meli ya mafuta katika Ghuba ya Oman mwezi Mei na Juni - madai ambayo Iran inapinga vikali.
Iran pia ilidungua ndege ya upelelezi ya Marekani isiyokuwa na rubani katika anga lake katika hali ya kutatanisha.
Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yaliripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz - kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza.
Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu maafisa wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya mafuta iliambiwa isimame katika maji ya Iran yaliyopo karibu ,lakini ikarudi nyuma na kuondoka baada ya onyo kutolewa na mele ya jeshi ya Uingereza.
HMS MontroseHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMeli ya kijeshi ya Uingereza HMS Montrose imeripotiwa kuifukuza mbali maboti ya Iran
Iran imekuwa ikitishia kulipiza kisasi kufuatia kushikiliwa kwa moja ya meli zake za mafuta ambayo ilitekwa karibu na ibraltar wiki iliyopita.
Hivi karibuni Iran ilitangaza kuvunja mkataba kuhusu kiwango cha urutubishaji wa madini ya urani, mkataba uliowekwa mwaka 2015.
Naibu waziri wa mambo ya nje, Abbas Araqchi amesema Iran bado taifa hilo linataka kutekeleza mkataba huo lakini ameyashutumu mataifa ya Ulaya kwa kutotimiza wajibu wao.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje Mohammad Javad Zarif amesema mazungumzo kuhusu silaha yatafanyika ikiwa vikwazo vitaondolewa.

Wednesday, July 17, 2019

Utafiti: Vikombe vya hedhi vinaweza kumstiri mwanamke sawa na sodo

Woman holding a menstrual cup and a tamponHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wanawake sasa wamehakikishiwa kuwa vikombe vya hedhi havivuji, wanasema wataalamu waliofanya utafiti wa kwanza wa kisayansi kuhusu bidhaa hiyo ya kujisitiri ukiwa na hedhi.
Vikopo vya hedhi havifyonzi damu bali hukusanya damu ya hedhi. 
Vinaingizwa ukeni sawa na sodo aina ya tampon lakini vinaweza kutumika tena baada ya kusafishwa.
Japo zimepata umaarufu uchunguzi umebaini kuwa ufahamu wa wanawake kuhusu vikopo hivyo vya hedhi uko chini sana.
Utafiti huo uliochapishwa katika Jarida la matibabu la Lancet ulichunguza tafiti 43 zilizohusisha wanawake na wasichana 3,300 wanaotoka nchi tajiri na masikini. 
Baadhi ya masuala yaliojitokeza katika utumizi wa vikopo hivyo ni kuwa wengine walihisi uchungu, tatizo la kukiweka au kukitoa na pia kuvuja.
Sanitary productsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Lakini uchunguzi huo ulibaini hapakua wa na tatizo lolote.
Matokeo ya tafiti 13 ilionesha kuwa 70% ya wanawake walitaka kuendelea kutumia vikombe vya hedhi walipogundua jinsi zinavyofanya kazi.
Tafiti nne zilizohusisha wanawake 300 zimefanywa ili kulinganisha utendakazi wa vikombe vya hedhi na soda za kawaida zinazotumika mara moja na kutupwa .
Tatu kati ya tafiti hizo zilibaini kuwa sodo huvuja ikilinganishwa na vikombe hivi na moja ilisema ni nadra kuona vikombe hivi vikivujisha danmu vikitumiwa vizuri. 
Vinafanya vipi kazi?
Vikopo vya hedhi vinatengenezwa kutokana na vifaa laini kama vile raba na silicone.
ikiingizwa ukeni huzua damu kumwagika nje. 
Husaidia kukusanya hedhi nyingi kuliko vile tampon ama pedi inavyofyonza damu lakini vinahitaji kutolewa na kusafishwa mara kwa mara.
Kuna aina mbili ya vikombe hivi- kuna vile vinavyowekwa ukeni lakini sio mbali sana na huwa na muundo wa kengele na kuna vile vinavyowekwa katika shingo ya uzazi na mara nyingi hutumiwa kama aina moja ya uzazi wa mpango.

Jinsi ya kutumia

Tafuta kikopo kinachoendana na umbo wa mwili wako. Umbo hilo halihusiani kwa vyovyote na kiwango cha hedhi unayopata. 
Hakikisha kikombe unachotumia ni kisafi. 
Kim na Amanda wanaelezea vikopo vya hedhi vinavyofanya kazi
Kunja kikombe hicho kisha uingize ukeni na moja kwa moja kitajifungua na kuzua kutoka kwa damu.
Ukitaka kukitia finyilia sehemu ya chini ya kikombe na kuachilia kutatoka.
Mwaga chooni uchafu ulioko ndani kicha kisafishe kikombe vizuri na kukikausha ili uweze kukitumia tena. 
Ni vigumu kufanya maamuzi?
Kuna visoda kila aina lakini kikombe cha sio vingi.
Itamchukua mwanamke muda mrefu kabla ajisikie huru kukitumia.
Debra Holloway, daktari bingwa wa masuala ya afya ya uzazi amesema gynaecology nurse: "kuna bidhaa nyingi sana sokoni ni vyema kujaribu modo baada ya nyingine hadi upate ile utakayokufaa."
Wataalamu wanasema kile kitu wanawake wanatumia kujisitiri wakati wa hedhi ni uamuzi wa kibinafsi lakini wanahitaji kushauriwa kwa kupewa maelezo yatakayowasidia kufanya uamuzi wa busara.

Tuesday, July 16, 2019

Air Tanzania: Faida ikoje baada ya kufufuliwa shirika la ndege Tanzania?

Wiki hii shirika la ndege nchini- Air Tanzania linaidhinisha njia mpya ya usafiri - jambo linalotazamwa kuwa fursa ya ukuwaji linapokuja sula la usafiri wa abiria.
Rais John Pombe Magufuli aliahidi kwamba shirika hilo litaimarishwa na ndege mpya kununuliwa mara baada ya kuingia madarakani.
Tanzania, kama ilivyo kwa nchi nyingine kama Zambia, Zimbabwe, Nigeria na Uganda, imelifufua shirika lake la ndege, ama kama lijulikanavyo, Air Tanzania.
Uwekezaji mkubwa umefanywa mpaka sasa katika kulifanikisha hilo.
"Shirika letu la ndege lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa na ndege moja tu tena ilikuwa inafanyiwa matengenezo mara kwa mara, soko la ATCL lilishuka sana hadi kufikia asilimia 2.5.
Lakini sasa tumenunua ndege 7, na nyingine kubwa aina ya Boeing 787-8 Dreamliner itakuja mwaka 2020", alisema Rais Magufuli mwaka jana 2018 katika hafla ya kuipokea ndege mpya ya Tanzania.
AIR TANZANIAHaki miliki ya pichaIKULU
Image captionRais Magufuli akiwa ndani ya Air Tanzania mnamo 2018

Mambo yako vipi kwa Air Tanzania hii leo?

Mkurugenzi mtendaji wa Air Tanzania Ladislaus Matindi anasema shirika la ndege linapanuka, lakini sio hilo tu ila pia linadhihirisha namna shirika hilo lilivyopiga hatua katika suala la hisa katika soko.
Wakati Air Tanzania likianza, Matindi anaeleza kwamba lilikuwa linadhibiti 2% pekee ya hisa hiyo ya soko.
Precision na Fast Jet zikishikilia sehemu kubwa ya soko wakati huo. Kufikia sasa mkurugenzi huyo mtendaji anasema shirika hilo limesogeza udhibiti kwa zaidi ya 75%.
Akizungumza na BBC, Matindi ameeleza kwamba ufanisi huo umetokana na namna washindani wao walivyokuwa wakihudumu.
Kampuni ya ndege ya Precision ilitumia ndege ndogo na kusafiri katika maeneo machache, Fast jet ambayo haipo sokoni kwa sasa, anasema mbinu waliokuwa wakitumia ya safari za gharama ndogo ni ngumu kuimudu katika mataifa ya Afrika.
usafiri wa ndegeHaki miliki ya pichaAFP
Licha ya kwamba ni mbinu inayoonekana kulifaa soko la maeneo masikini, Matindi anafafanua kuwa kiwango cha watu wanaosafiri kutoka maeneo hayo haizidi 2% ya wanaosafiri kwa ndege.
Ili kupata ufanisi wa mbinu hiyo, 'ni lazima uwe na idadi kubwa ya wateja, ili ndege ijaye saa zote, na kuwe na mzunguko mkubwa wa safari hizo' anasema.
Anaeleza kwamba taswira nchini Tanzania ni kwamba idadi kubwa ya watu wako radhi kusafiri safari ndefu kwa basi, kwasababu hawawezi kumudu gharama za tiketi ya ndege.
Hatahivyo anatazama nafasi kwa shirika la ndege la Air Tanzania kutokana na kwamba idadi ya watu walio na kipato cha wastani inaongezeka nchini, na hilo anasema ni fursa kubwa kwa shirika hilo.
Hususan katika msimu kama huu wa sasa kunakoshuhudiwa wasafari wengi, hiyo inamaanisha kwamba shirika linafanikiwa kuuza tiketi za viti vyote katika ndege zinazosafiri za shirika hilo.
Air Tanzania

Air Tanzania ina ndege ngapi?

Shirika la Air Tanzania lina ndege saba, baada ya kununuliwa ndege sita chini ya mpango wa kufufua shirika hilo lililoanzishwa mwaka 1977.
Kuna Bombardier DASH8 Q400 tatu, mbili ambazo zilifika Tanzania Septemba 2016 na moja Juni 2017; Bombardier CS300 mbili na Boeing 787 Dreamliner ambazo zilitua Tanzania kati ya mei na Julai 2018.
Shirika hilo lilikuwa na Bombardier DASH8 Q300 moja ambayo ilikuwa ikihudumu tangu 2011.
Air Tanzania inamilikiwa asilimia mia moja na serikali kama ilivyo kwa mashirika ya ndege kama Ethiopia.
Kama mashirika mengine ya ndege katika bara la Afrika yalioshindwa kupata ufanisi, Air Tanzania kadhalika iliathirika kutokana baadhi ya mengine, shinikizo la soko.
Afisa mkuu mtendaji wa Air Tanzania anaeleza kuwa kipindi hicho kigumu kilitokana na utovu wa nidhamu ya biashara, akitaja mfano wa wakati ndege ikiwa angani, waziri aliyetarajiwa kuabiri ndege hiyo akachelewa, ndege inalazimishwa kurudi.

Monday, July 15, 2019

Donald Trump ashutumiwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya wabunge wa Democratic

AOC, Rashida Tlaib and Ayanna PressleyHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRashida Tlaib (kati), akiwa na Alexandria Ocasio-Cortez (kushoto) na Ayanna Pressley (kulia)
Rais wa Marekani Donald Trump ameshutumiwa kwa ubaguzi wa rangu baada ya kundika ujumbe kwenye twitter akiwashambulia wabunge wanawake wa chama cha Democratic.
Amedai kuwa wanawake hao "wamewasili kutoka mataifa ambayo serikali zake ni majanga matupu", kabla ya kupendekeza "warudi walikotoka".
Baada ya hapo alisema kuwa spika Nancy Pelosi "atafurahi sana kuwashughulikia kwa haraka mipango ya safari ya bure".
Haya ni wiki moja baada ya Bi Pelosi kukabiliana kwa maneno na "kundi hilo", la wabunge wasio watu weupe wa mrengo wa kushoto wa chama cha Democratic.
Kati ya wabunge hao wanne, watatu - Alexandria Ocasio-Cortez, Rashida Tlaib na Ayanna Pressley - walizaliwa na kulelewa Marekani, huku wanne, Ilhan Omar, alihamia Marekani alipokuwa mtoto.
Bi Ocasio-Cortez alizaliwa mjini Bronx - New York, kiasi cha maili 12 kutoka hospitali ya Queens alikozaliwa Trump mwenyewe.
Rais Trump amesema nini?
Katika msururu wa ujumbe kwenye twitter, Trump amewashutumu wabunge hao kwa kumshutumu yeye na Marekani kwa "ukali".
Aliandika: "Inavutia kuona wabunge wa Democratic 'wanaotaka maendeleo' ambao waliwasili kutoka nchi ambazo serikali zake ni majanga matupu, zilizo mbaya zaidi, zilizo na kiwango kikubwa cha rushwa, na zisizojiweza kokote duniani (iwapo ni serikali zilizokuwa zinafanya kazi) sasa wakizungumza kwa ukali wakiwaambia watu wa Marekani, taifa kubwa na lenye nguvu duniani, namna tunavyostahili kuiendesha serikali yetu.
"Kwanini wasirudi kusaidia kuyarekebisha mataifa yaliosambaratika na yaliogubikwa kwa uhalifu wanakotoka. Alafu warudi watuonyeshe namna inavyostahili kushughulikiwa.
"Maeneo hayo yanhitaji usaidizi wenu sana, mungeondoka haraka sana. Nina hakika Nancy Pelosi atafurahi sana kuwashughulikia mipango ya safari ya bure!"
TrumpHaki miliki ya pichaAFP
Hakuwataja moja kwa moja wabunge wanawake waliokuwa akiwazungumza.
Hatahivyo, kutokana na kumtaja Bi Pelosi imedhaniwa pakubwa kwamba anamaanisha Bi Ocasio-Cortez, Bi Tlaib, Ms Pressley na Bi Ms Omar.
Katika wiki iliyopita, Pelosi amekabiliana kwa maneno na Bi Ocasio-Cortez, aliyemshutumu kwa kuwashutumu wanawake wa rangi kufuatia tofauti kati ya Democrat kuhus mswada wa usalama wa mpakani.

Kauli hiyo imepokewaje?

Bi Pelosi, spika wa bunge, amenukuu ujumbe wa Trump na kutaja maneno yake ya "kibaguzi".
"Wakati @realDonaldTrump anawaambia wabunge wanne wa Marekani warudi nchini mwao, anthibitisha mpango wake wa 'Make America Great Again' unahushu kuifanya Marekani liwe taifa ka watu weupekwa mara nyingine," alisema.
"Utofauti wetu ndio nguvu yetu na umoja wetu ndio nguvu zetu," amesema.
Presentational white space
Bi Tlaib, mbunge wa Michigan 13th district, alituma ujumbe akitaka kura ya kutokuwana imani na Trump iidhinishwe.
"Unataka jibu kwautovu wa sheria na kushindwa kwa rais ? Yeye ndiye janga. Mitazamo yake ndiyo janga, anahitaji kura ya kutokuwana imani naye" aliandika.
Bi Ocasio-Cortez alimtumia Trump ujumbe: "zaidi ya kutokubali kuwa Marekani imetuchagua, huwezi kukubali kwamba hatukuogopi."
Presentational white space
Bi Omar alimwambia rais kwamba "anapalilia utaifa wa watu weupe kwasbaabu una hasira kuwa watu kama sisi wanalitumikia bunge na kupambana dhidi ya ajenda yako ya chuki".
Kadhalika alimuita "kiongozi mbaya, mfisadi mkubwa na kiongozi asiyeweza kuwajibika tuliyewahi kumuona".
Na Bi Pressley alituma picha aliyonasa ya ujumbe wa Trump akiongeza: "HIVI ndivyo ubaguzi wa rangi ulivyo Sisi ni demokrasia ilivyo."
Wanachama wa Democratic wanaowania uteuzi wa urais pia walimshutumu Trump. Seneta Elizabeth Warren alisema "kauli chafu" ni "shambulio la kibaguzi"
Bernie Sanders pia alimshutumu Trump kwa ubaguzi
Presentational white space
Wabunge wachache wa Republican walituma ujumbe moja kwa moja ila binti yake John McCain anayekiunga chama hicho mkono Meghan McCain -alisema: "Huu ni ubaguzi wa rangi."
Wachambuzi wengine pia walishutumu katika mitandao ya kijamii