Friday, July 12, 2019

Uzazi wa mpango: Uhaba wa dawa wachangia idadi ya watu Uganda kuongezeka kwa zaidi ya 3% kwa mwaka

afya ya uzazi ugandaHaki miliki ya pichaJONATHAN TORGOVNIK
Uganda ina uhaba wa dawa za kupanga uzazi na kuzuia mimba - kingamimba kama zinavyofahamika kwa umaarufu. 
Wakuu wa afya na asasi za kijamii wanahofu kwamba sasa wanawake na wasichana baleghe wanakabiliwa na kitisho cha kushika mimba bila kutaka. 
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kizazi cha Uganda, kufika mwaka huu 2019, kinakaribia watu milioni 46, kikikua kwa zaidi ya 3% kila mwaka. 
Uhaba wa kingamimba ni tisho kwa mlipuko wa kizazi, mfumo wa afya na pia dhidi ya uchumi wa nchi.
Tangu Mei mwaka huu, dawa kadha za kuzuia mimba, zikiwemo Sayana, ya kujipiga sindano; Jadelle na Implanon, za kupandikiza; na vidonge vya dharura, zimeadimika. 
wanawake na afyaHaki miliki ya pichaJONATHAN TORGOVNIK
Afisa mhusika katika wizara ya afya, Dk Placid Mihayo, amekiri na kunukuliwa kwamba kweli kuna upungufu, na hivi wanazieneza upya - ikimaanisha kwenye nyingi hupunguzwa na kupelekwa zinako-kosekana. 
Sababu ya upungufu huo ni pesa hakuna. 
Kuna pengo kubwa chini ya makisio ya Wizara ya Afya ambayo inalipia nusu tu ya madawa yanayohitajika nchini, na kutoa wito mabia wasaidie kifedha. 
Tabia tegemezi inalaumiwa kwa athari mbaya juu ya afya ya uzazi.
Miongoni mwa athari hizo, mkurugenzi mtendaji wa asasi moja ya kijamii, Coalition of Health Promotion and Social Development, au kifupi, mseto wa HEPS-Uganda, Denis Kibira anasema: 'Kitu cha kwanza kabisa, ni mimba ziso-kusudiwa. 
'Ukiwa na mimba ziso-kusudiwa, ina maana hatufikii lengo la maendeleo ya milenia, la kupunguza vifo vya mama-wajawazito kwa thuluthi mbili; na kingamimba ndio njia moja wazi kabisa ya kufanikisha hilo. 
afya ya uzazi ugandaHaki miliki ya pichaJONATHAN TORGOVNIK
Upungufu wa kingamimba unamaana mimba ziso-kusudiwa zitaendelea kuwa gharama juu ya mfumo wa afya na pia kuugharimu uchumi wa nchi' anasema Dennis Kibira.
Zaidi ya 75% ya watu milioni 45 wanaishi vijijini Uganda, wengi wao wanawake wa marika ya kuweza kuzaa. Wanahitaji dawa hizo.
Je watazipata vipi?
'Itawapasa kulipa, na unajua matumizi kutoka mfukoni ni ghali mno Uganda. Hivyo wengi wakaazi wa vijijini wanaohitaji dawa hizo itabidi wawe bila' anaeleza Kibira.
Mseto wa HEPS-Uganda unafanya kazi katika wilaya 16 nchini, kwa miradi ya afya, mkiwemo uzazi wa majira. 
Na ukosefu huo, inasema HEPS, ni tisho kwa mripuko wa kizazi kinachokua kwa zaidi ya 3% kila mwaka nchini.

No comments:

Post a Comment