
Iran inasema kuwa imekamata meli ya kigeni ya mafuta na wafanyikazi wake 12 ikisafirisha ''kimagendo'' mafuta kati eneo la Ghuba siku ya Jumapili.
Runinga ya kitaifa imewanukuu maafisa wa jeshi la majini wakisema kuwa meli hiyo ilikuwa na lita milioni moja ya mafuta.
Haijathibitishwa ikiwa meli hiyo ni ile inayomilikiwa na Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE- ambayo ilipoteza mawasiliano ikiwa katika bahari ya Strait of Hormuz Jumapili.
Mapema wiki hii Iran ilisema kuwa iliisaidia meli iliyoharibika katika eneo lake bila kutaja jina la meli hiyo, na kuongeza kuwa iliivuta kutoka majini kwenda kuikarabati baada ya ''kupokea ombi al usaidizi''
Hali ya taharuki imekuwa ikishuhudiwa katika eneo la Ghuba tangu Marekani ilipoiwekea upya vikwazo vilivyolenga sekta yake ya mafuta na kujiondoa katika mkataba wa kimataifa wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015.

Katika kujibu hatua hiyo, Iran ilitangaza mwezi Julai kuwa imeongeza kiwango cha urutubishaji wa madini ya urani yaliyowekwa kwenye makubaliano hayo.Nchi hiyo imesisitiza kuwa haijaribu kutengeneza silaha za nyukilia.
Katika mahojiano ya televisheni siku ya Jumatatu, Bwana Zarif amesema kwenye televisheni ya NBC kuwa nafasi ya mazungumzo ipo wazi'' ikiwa Marekani itaondoa vikwazo.
Raisi wa Marekani Donald Trump amesema Marekani ''imepiga hatua'' na Iran na kuwa hawakuwa ''wakitafuta kuubadili utawala'', ingawa alisisitiza kuwa nchi haiwezi kutengeneza silaha za nyukilia na haiwezi kujaribu makombora ya masafa marefu.
Mapema mwezi Mei, Trump aliweka shinikizo zaidi kwa Iran kwa kuidhinisha upya marufuku kwa matiafa yanayonunua mafuta kutoka kwa Iran.
Hatua hiyo ilinuiwa kusitisha kipato kikuu kwa serikali ya Iran.

Kwanini Iran imeongeza viwango vya urutubishaji?
Rais wa Iran Hassan Rouhani alitangaza kuwa nchi yake inarudi nyuma katika ahadi zake katika makubaliano hayo.
Hii ikiwa ni pamoja na kutotiii sheria kuhusu akiba yake ya urutubishaji mdogo wa madini ya Uranium kiwango kilichowekwa kikwa ni - 300kg na tani 130 - na kusitisha uuzaji wa akiba ya ziada katika mataifa ya nje.
Rouhani pia aliyapatia mataifa hayo ya Ulaya siku 60 kulinda mauzo ya mafuta ya Iran. Iwapo yatashindwa kufanya hivyo , Iran itakiuka masharti ya urutubishaji Uranium na kusitisha uundwaji upya wa kinu cha Arak, ambacho mafuta yake yaliotumika yana plutonium yalio na uwezo wa kuunda mabomu.
Marekani imekuwa ikiilaumu Irana kwa kuhusika na mashambulio dhidi ya meli ya mafuta katika Ghuba ya Oman mwezi Mei na Juni - madai ambayo Iran inapinga vikali.
Iran pia ilidungua ndege ya upelelezi ya Marekani isiyokuwa na rubani katika anga lake katika hali ya kutatanisha.
Maboti ya Iran yaliyosheheni silaha yaliripotiwa kujaribu kuzuwia safari ya meli ya mafuta ya Uingereza katika eneo la kuwa maji la Strait of Hormuz - kabla ya ya kufukuzwa na meli ya kikosi cha majini cha Uingereza.
Taarifa za vyombo vya habari zimenukuu maafisa wa Marekani wakisema kuwa meli hiyo ya mafuta iliambiwa isimame katika maji ya Iran yaliyopo karibu ,lakini ikarudi nyuma na kuondoka baada ya onyo kutolewa na mele ya jeshi ya Uingereza.

Iran imekuwa ikitishia kulipiza kisasi kufuatia kushikiliwa kwa moja ya meli zake za mafuta ambayo ilitekwa karibu na ibraltar wiki iliyopita.
Hivi karibuni Iran ilitangaza kuvunja mkataba kuhusu kiwango cha urutubishaji wa madini ya urani, mkataba uliowekwa mwaka 2015.
Naibu waziri wa mambo ya nje, Abbas Araqchi amesema Iran bado taifa hilo linataka kutekeleza mkataba huo lakini ameyashutumu mataifa ya Ulaya kwa kutotimiza wajibu wao.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje Mohammad Javad Zarif amesema mazungumzo kuhusu silaha yatafanyika ikiwa vikwazo vitaondolewa.
No comments:
Post a Comment